Mtambue Rafiki adui

Marafiki wa kweli Dhidi ya Marafiki bandia

Mtambue Rafiki adui

Wiki iliyopita nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu wa thati aitwaye Afifa. Alionekana kuwa na wasiwasi kwa sababu kuna msichana kwenye mtaa wake ambaye hujifanya rafiki siku moja na siku nyingine ni mbaya. Hiyo kwangu si vizuri kwa sababu ninawajua marafiki wanapaswa kuwa na upendo na wanao kuunga mkono. Kwangu msichana huyu alionekana kama "Rafiki adui". "Rafiki adui" ni mtu anayejifanya kuwa "rafiki" yako lakini kwa kweli anatenda kama adui yako. Dada yangu mkubwa alinifunza zamani jinsi ya kuwagundua kwa hivyo nikamfunza Afifa jinsi ya kufanya hivyo pia. Hivi ndivyo nilivyomwambia:

Mtumiaji Dhidi ya Mtoaji

Rafiki adui hujifanya kuwa rafiki yako wakati anahitaji kitu kutoka kwako. Akipata hivi tu, hajali kukuhusu tena. Siku moja unamsaidia na kazi ya nyumbani na wakati mwingine unaskia anakuita majina wakati hauko. #notcool Marafiki wa kweli ni wale wanaotoa na kushiriki. Wana furahia kutoa bila kutarajia kupata chochote. Wako hapo kwa ajili yako wakati wa nyakati nzuri NA nyakati mbaya.

Msababisha shida Dhidi ya Mfano mzuri

Hadharani Rafiki adui hujifanya kana kwamba hakujui lakini faraghani atakuomba ufanye mambo mabaya kwa niaba yake katika jina la "urafiki"... kama vile kuiba pesa kutoka kwa wazazi wako ili umnunulie muda wa maongezi ya simu. Upande ule mwingine rafiki wa kweli hukufanya ujihisi mtu wa maana wakati wowote anapokuona. Hakuombi pia ufanye mambo ambayo yanaweza kukuweka taabani. Badala yake anakuhimiza kuwa mtu mzuri na ufanye mambo mazuri.

Mkosoaji Dhidi ya Anayekutia moyo

Rafiki adui hukukosoa - utasikia mara kwa mara akisema "Unakera sana". "Hujuia hii hata kidogo, sijui kwanini nilikuomba msaada" au anakukosoa unavyoonekana..."Nywele yako ni mbaya ikiwa hivyo, ibadilishe"

Marafiki wa kweli hufanya kinyume chake. Wanakuhimiza na kukuambia mambo mazuri. Unapochukua muda nao hutoki hapo ukijishuku. Badala yake unatoka hapo ukihisi umejawa na nguvu na ujasiri.

Afifa alifurahi sana nilivyoshiriki naye yale niliyoyajua. Aligundua msichana huyo alikuwa Rafiki adui na akafanya uamuzi wa kujisimamia na kuwa tu karibu na watu wazuri. Ninajivunia yeye kwa kutumia sauti yake na kuwa na ujasiri. Sasa hana matatizo yoyote ya urafiki.

Ninafuraha pia alikuja kwangu kupata ushauri na nilikuwa na nafasi ya kumsaidia rafiki yangu. Ninapenda kuwa rafiki mzuri kwa hivyo kabla ya kukata simu nilimwambia jambo lingine moja: "Afifa kumbuka kila wakati kwamba nitakuwa rafiki yako na nitakuwepo wakati wowote utakaponihitaji"