Ongea. Pata kile unahitaji.

Tulianza timu ya wasichana pekee

Ongea. Pata kile unahitaji.

Habari Wana Springster!

Jina langu ni Naobi na nahudhuria shule ya wasichana na wavulana. Tangu nilipokuwa mdogo nilipenda kucheza kandanda na ndugu zangu. Lakini nilipojiunga na sekondari, wakati wa michezo wavulana walikwenda nje kucheza kandanda na wasichana walilazimika kubaki darasani na kusoma. Nilipomwuliza mwalimu wangu sababu za wasichana kutoweza kucheza kandanda, alijibu kuwa "una machafuko mengi" na hivyo wasichana hawataufurahia.

Fikiria hilo! Wasichana pia wana nguvu, na tunaweza kufanya chochote ambacho wavulana wanafanya. Hatufai kubaki ndani na kufanya shughuli tulivu. Kuwa mwenye shughuli na kujaribu mambo mapya ni muhimu.

Baada ya shule nilizungumza na wasichana kadhaa kuhusu wazo langu, na walikuwa wakiwaza mambo sawa! Tunaamini kuwa wasichana wana haki sawa na wavulana, tulichohitaji kufanya ni kuungana, kuongeza sauti zetu na kuwa na msimamo. Kuna nguvu katika watu wengi!

Kukusanya wachezaji

Tulihitaji njia ya kufanya sauti zetu kusikika, hivyo kwanza tulikusanya kila mtu kwa majadiliano madogo ili kuhakikisha sisi sote tulikuwa na lengo sawa ndani yetu. Ni muhimu sana kuonekana kama kundi moja wakati wa maamuzi. Baadaye tulikwenda uwanjani ili kucheza kandanda ya kirafiki. Ilikuwa ya kusisimua sana!

Fanya mambo kutendeka

Siku iliyofuata habari zilienea kuhusu shughuli zetu na ilikuwa habari njema. Wiki baada ya nyingine, wasichana zaidi waliendelea kujiunga nasi baada ya shule. Unapaswa kutenda jambo ili kuonyesha watu kwamba unachukulia malengo yako kwa uzito. Wanasema vitendo ni muhimu kuliko kuongea. Kwa matendo yetu tulionyesha kwamba wasichana pia wanaweza kucheza michezo. Na watu waliweza kujionea wenyewe.

Kufikia lengo letu

Tuliongeza sauti zetu. Tulifanya tendo na kuonyesha nia yetu. Sasa ulikuwa wakati wa kufanya ombi letu. Tuliamua kuandika barua kwa mkuu wa shule na kumweleza umuhimu wa kandanda na michezo kwetu. Mimi pamoja na wasichana wengine wawili tulipeleka barua hizo na kuomba ikiwa tunaweza kufanya rasmi timu yetu ya baada ya shule. Tulitaka kocha mzuri na mazoezi sawa na wavulana. Dhania nini? Alisema ndiyo! Alitambua shauku na ushupavu wetu na alipendezwa sana na sisi.

Sasa tumeshinda michuano kadhaa shuleni. Na tumejidhihirisha kuwa tunapoungana kama wasichana, kuchukua hatua na kusema mawazo yetu, tunaweza kuwa na ushawishi juu ya maamuzi yanayotuathiri.