Kuwakilisha wasichana wangu wote!

Tunaweza pia kuwa viongozi

Kuwakilisha wasichana wangu wote!

Je kuna mtu ashawai kukwambia kwamba wavulana tu ndio wanaweza kuwa viongozi? Au wasichana wanafaa kuketi kando na kuwa kimya? Basi, ikiwa umeambiwa hivo maisha yako yote niko hapa kukujulisha sio kweli!

Jina langu ni Selma na mimi huenda shule ya mseto. Kila mwaka kuna nafasi wazi kwenye Baraza la Wanafunzi. Hili ni kundi la wanafunzi wanaoshikilia nafasi za uongozi na wanawakilisha wanafunzi wengine wote wakati maamuzi makuu yanafanywa. Pia, kama kuna jambo wanafunzi wengine hawajafurahia, Baraza la Wanafunzi linaweza kupeleka visa hivyo kwa Mwalimu Mkuu.

Hapo awali nafasi zote za baraza la wanafunzi zilishikiliwa na wavulana. Wasichana wengine waligombea lakini daima walichagua wavulana. Baadhi ya wavulana walikuwa viongozi wazuri lakini wakati mwingine sisi wasichana tulipotoa masuala yaliyotugusa sisi ilionekana kana kwamba hakuna kilichofanyika na hakuna mtu aliyesikiliza. Kitu flani kuhusu hilo hakikuwa sawa kwangu. Wasichana na wavulana ni sawa na sauti zote zinastahili kusikilizwa.

Mara nilipokuwa mwafaka niliamua kugombea nafasi katika baraza, kwa sababu wakati ulikuwa umefika mtu awakilishe wasichana. Mmoja wetu alihitajika kusonga mbele na kuwa sauti ya wasichana wengine ambao hawakuwa na nafasi ya kujieleza wenyewe. Na huyo mtu alikuwa MIMI!

Nilipiga kampeni kwa bidii na hatimaye nilipata sehemu! Mwanzoni, kuwa msichana wa pekee kuliogofya lakini nilijua nilihitaji kuwa jasiri kwa sababu wasichana wengine wote walikuwa wananitegemea. Baada ya mkutano wetu wa kwanza wavulana waligundua kwa haraka kwamba wasichana wanaweza kufanya mchango mkubwa pia mawazo ni bora wakati wasichana na wavulana wanapofanya kazi pamoja. Sisi wasichana tuna njia ya kipekee ya kufikiria na hivyo wakati maamuzi yanafanywa ni muhimu tuonekane na kutoa maoni yetu. Huwezi kusubiri daima mwaliko wa kuzungumza, unapaswa kuchukua fursa.

Kwa hivyo kumbuka Springsters – ulichonacho cha kusema ni muhimu na wasichana wengine wanakutegemea, hivyo jiamini na ufuate kilicho chako.