Simulizi yangu ya kuchekesha ya hedhi

Sote tuna nyakati za aibu

Simulizi yangu ya kuchekesha ya hedhi

Enyi Springsters,

Nakumbuka siku ya kwanza nilipopata hedhi yangu. Nilikuwa na miaka 12 na marafiki zangu na mimi tulikuwa tumeketi Jumamosi kwenye bustani. Kika kitu kilikuwa sawa hadi niliposikia maumivu ya tumbo. Sikuona vyoo karibu hivyo niliamua kupuuza.

Maumivu ya tumbo yaliendelea hivyo ilinibidi niinuke na nilianza kuulizia kila mtu choo kiko wapi.

Manuel, rafiki yangu, aliniona nimeshika tumbo langu na kuuliza ikiwa nataka kwenda chooni. Nikiwa nimeshikwa na haya kubwa nilikubali kwa kutikisa kichwa changu. Kabla ya kujua, alinipandisha kwenye baiskeli yake na kuanza kuendesha kuzunguka bustani akitafuta choo. Unaweza kufikiria jinsi gani ilivyochekesha? Mimi nikikaribia kufa kwa aibu na Manuel akipiga kelele, "Choo, choo, tunahitaji choo."

Wakati nilipokuwa nashuka kwenye baiskeli tayari nilikuwa nimechelewa sana. Niliaangalia chini kwenye suruali yangu na nilikuwa nimeanza hedhi yangu! Ningekuwa yule wa zamani ningekuwa nimejionea aibu sana na kutoa machozi lakini sikufanya hivyo. Nimesoma simulizi nyingi za hedhi kwa Springster na hedhi ni kawaida! Manuel kwa haraka alinipa sweta yake nivae ili nipate kusitiri doa. Lilionekana kuwa kubwa kwangu nilipolivaa sisi sote tuliangua vicheko jinsi ilivyokuwa inaonekana.

Niliingia chooni ili kusafisha suruali yangu na kabla ya kutoka nje kukabiliana na marafiki zangu, nilitoa kitabu changu mfukoni cha ujasiri ambacho daima hukibeba. Nilitazama kwenye kioo na kuanza kusoma thibitisho zifuatazo:

  1. Hedhi ni kawaida, hakuna haja ya kuwa na aibu.
  2. Maoni ya watu kwangu hayanielezei mimi. Daima nitajiamini mwenyewe.
  3. Nina nguvu. Nina ujasiri. Mimi ni mrembo.
  4. Ninaweza kujisikia kuwa na wasiwasi na aibu lakini huyo sio mimi. Nina nguvu. Nina ujasiri. mimi ni mrembo

Nilisema kwa kurudia mpaka hofu yangu yote ikaondoka. Kuanza hedhi yako mbele ya watu sio sababu ya kupoteza ujasiri wako. Wakati wa aibu hauna haja ya kudumu milele. Jifunze kuachia na uzingatie vitu chanya!