Akina mama ni Springsters waliokomaa tu

Hao sio tofauti vile!

Akina mama ni Springsters waliokomaa tu

Nilikuwa katika darasa la Kiingereza siku moja shuleni na nikahisi kitu cha ajabu ndani yangu. Nikaangalia chini na nikagundua nilikuwa nimeanza hedhi nikiwa darasani. Lo! Kwanini darasani? Kwanini darasani mahali kila mtu yuko? Ninaelewa kwamba hedhi ni jambo la kawaida, lakini nilikuwa nikiona haya kidogo, kwa hivyo nikamwandikia mwalimu ujumbe na nikaupitisha kwa rafiki yangu ampatie. Wakati mwingine unapoona haya sana kuongea, kuandika barua kunaweza kuwa njia nzuri mbadala. Mwalimu alinipa tabasamu kwa siri na kisha akasema kwa sauti ya ukali “kila mtu aende nje kwa mapumziko ya dakika 10, Cinta bakia nyuma”. HA. Kila mtu alifikiria nilikuwa taabani lakini kwa kweli mwalimu wangu alikuwa akiniunga mkono.

Nilimwomba ushauri wa jinsi ya kuwaelezea wazazi wangu. Nilikuwa nikiona haya kwa sababu mama yangu na mimi hatuzungumzii sana kuhusu masuala ya kibinafsi. Hata hivyo, alinipa mtazamo mpya. Wanawake wote hupata hedhi na mama yangu ataweza kuelewa uzoefu wangu. Baada ya yote, alikuwa msichana mdogo pia.

Bi. Ndali alisema pia niongee na mama yangu wakati wa shughuli ya burudani anayofurahia. Kwa njia hiyo sisi wote tutakuwa tumetulia na mazungumzo yatakuwa rahisi. Nilipofika nyumbani kutoka shuleni nilimuuliza mama yangu tutengeze keki pamoja. Anapenda kuoka na tulipokuwa tukipamba keki hiyo nikamwelezea kuhusu siku yangu. Aliniunga mkono sana na akanikumbatia sana. Nilihisi nimetulia.

Sasa nina umri wa miaka 18 na mama yangu na mimi tuna uhusiano wa karibu sana na tunaweza kuzungumzia kitu chochote. Ninamwona mama yangu kama Springster aliyekomaa tu. Yeye huelewa kabisa ninachokipitia maishani na yuko hapa kunihimiza jinsi vile sisi Springsters hufanya. Tumepitia mambo sawa akikua kwa hivyo sina sababu ya kuogopa kuongea na yeye. Ninampenda na ananipenda zaidi!