Ni wakati wa kuongea!

Ikiwa kuna moto moyoni mwako unahitaji kuutoa

Ni wakati wa kuongea!

Mimi hupenda sanaa na vitambaa. Wakati wowote ninapochora ninahisi vizuri kana kwamba moyo wangu umejawa na furaha na shauku. Nilihisi ndani moyoni mwangu kwamba nitakuwa na kampuni yangu ya mitindo. Shule yangu haikuwa na masomo yoyote ya sanaa kwa hivyo nilifikiria kuhusu kufanya masomo ya kushona na kuchora baada ya shule ili kuboresha ujuzi wangu. Tatizo lilikuwa tu kwamba kila mtu katika nyumba yangu hufanya kazi katika mkahawa wa familia. Baba yangu husema tu "nina ndoto kubwa kwa ajili yako ya kufanya kazi kama keshia katika mkahawa." Baba yangu alikuwa na ndoto zangu lakini nilikuwa na ndoto zangu zingine. Sikujua jinsi ya kumwelezea. Binti yake wa pekee hakutaka kufanya kazi katika mkahawa wake.

Jioni moja baada ya kusoma makala kuhusu ujasiri kwenye Springster niliweza kuwa na ujasiri wa kutosha wa kumwelezea baba yangu nilitaka kuwa mwana mitindo. Ningetaka hii ingekuwa sehemu ya hadithi ambapo ninasema baba yangu alisema ndiyo na kila kitu kikawa sawa. Kwa bahati mbaya hakufurahi hata kidogo...Aliniuliza mamilioni ya maswali ambayo singeweza kujibu. Nilitoka huku nalia nikaenda chumbani mwangu, nilikuwa na huzuni sana kuhusu jinsi mazungumzo yalivyokuwa. Ndugu yangu mkubwa akaja kwa sababu alikuwa amesikia mazungumzo yote. Akasema “Mazzy unahitai mpango”. “Huwezi tu kumwendea baba bila wazo la kozi unayotaka kufanya au mifano ya nguo ulizounda. Unawezaje kumtarajia aamini unaitaka sana." Alikuwa na wazo zuri!

Kwa hivyo miezi iliyofuatia niliweka akiba na kukodisha mashine ya kushona na baada ya shule nilitengeneza skafu za shangazi zangu wote ili kuonyesha baba yangu kwamba nataka hii sana. Nikapata kozi ya kushona karibu na nyumbani ambayo ilimaanisha siku zingine ninaweza bado kufanya kazi mkahawani. Baada ya miezi 6 nilijaribu tena. Nilimrudia baba yangu na nikauliza tena na wakati huu alikubali kabisa!

Kwa hivyo Springsters wajifunze kutoka kwangu na wafuate hatua hizi wakati wanapoongea na wazazi kuhusu ndoto zao

  1. Chukua muda wa kupanga mazungumzo yako. Kuwa tayari na vipengele vyako vyote vya kuzungumzia na uvipitie na ndugu mkubwa kama unaweza.
  2. Unda mpango wa hatua na UANZE kuushughulikia ili uwe na kitu cha kuonyesha. Husaidia wakati wanaweza kuona unashughulikia ndoto yako.
  3. Jaribu na uongee nao wakati ni rahisi kwao. Iwapo mazungumzo hayaendi vizuri wakati wa kwanza usife moyo. Endelea na uwaulize vidokezo vya jinsi ya kuboresha wazo lako.

Ikiwa bado hauko sawa kuongea nao jaribu kuandika barua au kumuuliza mtu mzima aongee nao kwa niaba yako.