Nilifuata uchu wangu wa spoti na kuwa mlinda lango

Nilifuata uchu wangu wa spoti na kuwa mlinda lango

Nilipenda kandanda tangu mara ya kwanza mimi na mamangu tulipoupiga mpira kwenye uwanja wa nyuma ya nyumba yetu. Nilipokuwa mkubwa, nilijuinga na timu ya shule yangu na kuwa mlinda lango.

Wakati ambapo timu nyingine hulenga ili kufunga bao, muda husonga polepole kweli - ni haraka zaidi! Ndoto yangu ni kuwa mchezaji wa nchi yangu.

Wiki chache zilizopita, kulikuwa na mashindano ya kutafuta mlinda lango bora zaidi katika eneo letu na mshindi angepata fursa ya kuchezea timu ya eneo.

Nilitaka kujaribu kweli, lakini sikuwa na uhakika kuwa iwapo nilikuwa tayari kupiga hatua nyingine katika kandanda yangu. Nilikuwa na uoga mwingi wa kuomba usaidizi au kushiriki ndoto zangu na marafiki au wanafamilia wangu kwa kufiriki kuwa hawangelizingatia hili zaidi.

Mkufunzi wangu wa kandanda alikuwa mchezaji wa timu yetu ya taifa na pia alikuwa mwanamke. Ni shabiki mkubwa zaidi wa timu yetu - Nilijua kuwa atalipa suala langu uzito na hangenicheka kama walivyofanya baadhi ya wavulana. Nilitaka kumwuliza iwapo alifikiria kuwa niko tayari na ikiwa angenisaidia katika vipindi vyetu vya mazoezi shuleni ili niwe tayari kwa majaribio.

Nilitaka kuhakikisha kuwa nimekuwa tayari nilipomwomba usaidizi wake. Kwa hiyo, niliandika mambo niliyotaka kumwuliza kikamilifu na jinsi ya kumweleza ni kwa nini jambo hili ni la umuhimu sana kwangu.

Kisha nilianza kufanya mazoezi ya kuyasema nilipotembea kuelekea shuleni ili nisiweze kuchanganya maneno yangu.

Nilitaka kuwa dhahiri sana kwake na kumwomba maoni yake ya kweli - Siwezi kuimarika iwapo sijui sehemu ambazo ninaweza kuimarika.

Nilihakikisha pia kumweleza jinsi ninavyolipa suala hili uzito na kuwa sitakosa kipindi chochote cha mazoezi yetu jinsi nilivyofanya muhula uliopita.

Mkufunzi alifurahia kweli kunisaidia na hata alikuwa anaenda kuniweka katika nafasi ya mbele kwa ajili ya majaribio haya!

Alinipa pia maoni yenye usaidizi kweli - kama vile jinsi nafasi ya mkono wangu ilivyokuwa chini zaidi na kuwa nilihitaji kuimarisha mpigo wangu wa mpira.

Imani na usaidizi wake kwangu ilinikumbusha tu jinsi nilivyokuwa na uhakika kuwa hiki ndicho ninachotaka kufanya na kuwa nina talanta.

Alinisaidia kuimarisha imani yangu ya kuwaambia watu kuhusu ndoto zangu kwa kunikumbusha kuwa siwezi kudhibiti maoni ya watu wengine - lakini kuwa watu wanaweza kunishangaza na kuwa wenye msaada zaidi iwapo nitawapa fursa. Kisha niliwaeleza wazazi, ndugu na marafiki zangu kuhusu ndoto zangu - na ingawaje wengine walicheka kwa mara ya kwanza, kwa sasa wote wamependezwa na uamuzi wangu.

Mkufunzi, wazazi, ndugu na marafiki zangu wote walikuja kutazama majaribio yangu, wakinishangilia! Hatimaye nilikuwa mshindi katika mashindano pia. Ninafuraha zaidi nilitafuta usaidizi na kushiriki ndoto zangu!