Nafaa kuwa na marafiki wangapi?

Ubora kupita Wingi!

Nafaa kuwa na marafiki wangapi?

Hamjambo wasichana

Jina langu ni Taiba na nilipoenda sekondari kuwa katika kundi lilikuwa jambo kubwa sana. Kama hukuwa katika “kikundi” hukuwa bora.

Niliwaona watu wengi wakiwa bandia na wakifanya mambo wasiyoyataka kwa sababu walihisi haja ya kuwa katika kundi.

Lakini niko hapa kukuambia kwamba urafiki si kuhusu wingi, ni kuhusu ubora. Ina haja gani kuwa na marafiki 10 ikiwa hakuna atakayekuja kwenye sherehe yako ya siku ya kuzaliwa? Au hakuna anayejitolea kukusaidia unapohitaji usaidizi sana.

Najua tunakabiliwa shinikizo kubwa kukubaliwa, lakini kujitokeza na kuwa wewe mwenyewe ni bora zaidi! Niamini!

Unapokuwa wewe mwenyewe unavutia marafiki wa kweli na halisi, wanaokupenda wewe mwenyewe. Sio watu wanaotaka kuwa marafiki ili wakutumie. Kama rafiki yangu Jema. Yeye ni rafiki wangu wa dhati na wa pekee, na ninafurahi sana kuwa naye maishani mwangu. Huwa tayari kunisaidia ninapomhitaji. Hunisaidia na kazi ya nyumbani ya sayansi, tunaenda nyumbani pamoja, na tunalindana. Tunasoma hadithi za Springster pamoja. Yeye hata huninunulia zawadi bila mpangilio anapoenda sokoni. Sasa huyo ni rafiki wa kweli. Haniiti tu anapotaka kitu. Au kunionyesha kitu. Huzungumza nami kuhusu siku zake nzuri na mbaya! Ninajua kila kitu kumhusu na anajua kila kitu kunihusu.

Siwezi kamwe kubadilisha Jema na marafiki wengi. Yeye ni kama marafiki milioni moja! Na ninampenda kwa hilo.

Kwa hivyo Springsters, usizingatie idadi ya marafiki ulionao... Zingatia aina ya marafiki ulionao, na hakikisha ni wazuri!