Jinsi nilivyoweka akiba ya pesa za kujiunga na chuo cha usanidi

Jinsi nilivyoweka akiba ya pesa za kujiunga na chuo cha usanidi

Mimi nimekuwa ninapenda kompyuta kila wakati. Ninakumbuka nilipokuwa mdogo zaidi, tulikwenda na mamangu katika kazi yake ya ofisini na nikaona kompyuta kwa mara yangu ya kwanza - Nilivutiwa.

Mwalimu wetu wa sayansi ananisaidia kujifunza usanidi wa msingi wa kompyuta - isitoshe, nimetengeneza gemu ya kompyuta ya msingi mwaka huu. Sasa, ninataka kujiunga na chuo cha usanidi nitakapohitimu.

Nimetuma maombi ya ufadhili wa masomo, lakini kuna ushindani mkubwa zaidi, kwa hiyo ninahitaji kuweka akiba.

Sijui jambo la kwanza kuhusu kuweka akiba ya pesa! Kila wakati mamangu hupata njia za kuweka akiba - kama vile kwenda sokoni mwishoni mwa siku ili kupata bei bora zaidi au kusubiri wakati wa mauzo ili kutununulia nguo zozote mpya. Nilifurahi zaidi alipokubali kunisaidia kutengeneza mpango wa kuweka akiba.

Kwanza, ninaweka lengo langu na kisha ninaligawanya lengo hilo katika miezi ili kupata muda wa kulitimiza. Nilikuwa nimesalia na miezi 10 tu kabla ya kuhitimu, kwa hiyo nilipaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu.

Kisha, tulipitia gharama zangu na kuangazia vitu ninavyovihitaji kwa rangi ya manjano na vitu vya ziada kwa rangi ya samawati. Mboga na matunda ni rangi ya manjano, lakini kupata mlo wa nje jioni sokoni pamoja na marafiki si hitaji, ni kitu cha ziada, kwa hiyo ni rangi ya samawati. Kwa miezi michache ijayo, nitasitisha matumizi ya pesa kwenye vipodozi na nguo mpya.

Nilianza kufanya kazi za ziada za zamu katika kazi yangu ya mkahawani na pia kutafuta kazi za kutunza watoto mara moja baada ya wiki mbili kwa majirani zetu.

Nilikuwa na shughuli nyingi zaidi, lakini nilipata motisha kwa kufahamu kuwa zilikuwa za miezi 10 tu na kuwa nitaweza kufikia lengo!

Nilinunua kibubu kidogo ili nisiweze kushawishika kutumia akiba yangu. Sasa niliweka akiba ya mapato yangu yote yaliyotokana na kazi yangu ya mkahawani kwenye kibubu changu kidogo, kisha kiasi cha pesa za matumizi yangu ni kile nilichokipata kutokana na kazi za kutunza watoto. Hazikuwa pesa nyingi lakini nilikuwa sinunui vitu vipya, ningezitumia kwa vitu vyangu vyenye umuhimu zaidi.

Nilihakikisha pia kuweka pesa hizi mahali salama na sio tu juu ya meza yangu. Nilizificha kabisa nyuma ya kabati langu la nguo!

Mwishoni mwa miezi 10, nilifikia lengo langu! Nilipokea ufadhili wa masomo usio kamili jambo lililomaanisha kuwa nilibaki na kiasi kidogo cha pesa - zilikuwa habari njema zaidi kwa sababu sikujumuisha gharama ya vitabu vilivyohitajika katika kozi kwa hivyo niliweza kuvinunua kabla ya masomo kuanza.