Tenda kama msichana

Na uanze hatua na kufikia malengo ya maisha!

Tenda kama msichana

Iwe ni kurushiana ngumi, kufunga magoli au kurusha mpira kwenye pete - hatua ya kujaribu mchezo mpya inaweza kukusaidia ujenge ujasiri wako ndani na nje ya uwanja! Itakuasaidia upate marafiki, ugundue uwezo wako - hatua ya kujiunga na kikundi cha michezo inaweza kukusaidia ustawi katika nyanja zote katika maisha yako.

Wasichana hawa wanashiriki hadithi zao kwa nini kufanya mambo kama msichana kuna nguvu sana!

Nyah alijiingiza katika ndondi ili aweze kuwa anajilinda mwenyewe. Anapenda wazo kwamba ana ujuzi zaidi kuliko ndugu zake au wavulana shuleni. Hata aliwashinda katika mashindano kadhaa ya mchezo!

Ndondi imemfundisha Nyah jinsi ya kuwa na uzingativu, jinsi ya kuwa hatua moja mbele na pia jinsi ya kusema 'ha' wakati anapiga hatua. Inamfanya ajihisi mwenye nguvu! Sasa Nyah anahisi kuwa na uwezo katika kila kipengele cha maisha yake na anaweza kukwepa shida yoyote maishani kama jinsi tu anavyokwepa ngumi!

Timu ya mpira wa soka ya Zola hukutana kila Jumamosi na yeye hutamani sana kuwa nao. Kila wakati yeye au timu yake inapofunga goli wote wanashangilia - wanajiita 'Simba-Majike'. Hawajali kuingia katika matope na kutoa jasho - lakini kila wakati wamejawa na tabasamu katika nyuso zao.

Wakati mwingine atafanya mazoezi katika uwanja siku ya Jumapili pia, pamoja na yeyote aliyepo na anafurahia sana kuonyesha ujuzi wake. Anahisi ujasiri sasa kwamba amepata kufanya jambo analopenda. Sasa hata ameanza kuwafunza ndugu yake mdogo na marafiki zake jinsi ya kucheza.

Dede alitiwa motisha wa kucheza mpira wa kikapu na babake ambaye alikuwa mchezaji alipokuwa mtoto. Aliwaomba wazazi wake kila wakati wote kwamba anataka kujiunga na timu - na ingawa kwa mara ya kwanza walidhani sio wazo nzuri, alisisitiza na hatimaye wakamruhusu.

Amejiunga na timu ya mchanganyiko na ni mmojawapo wa wasichana wawili tu katika timu hiyo. Mara ya kwanza walimtania na kusema kuwa hawezi kuwafikia. Lakini alihakikisha kwamba anahudhuria kila kipindi cha mazoezi walichokuwa nacho na kuhusika katika kila nafasi aliyopata! Sasa yeye anaweza kuwazunguka wavulana kwa urahisi sana.

Je, kuna mchezo ambayo umekuwa ukitaka kujaribu? Kwa nini usimwalike rafiki yako na umshawishi mhusike. Na kama mtu yeyote atasema kuwa unacheza au kurusha kama msichana - mwambie asante! Kwa sababu wasichana wanaweza kurusha ngumi kwa nguvu.