Unaye besti ambaye hukusaidia?

Wangu walinisaidia kila wakati

Unaye besti ambaye hukusaidia?

Habari! Naitwa Amina, na naishi mtaa mdogo karibu na jiji kubwa. Nina bahati nzuri ninao marafiki wa karibu ambao ni Neema na Mariam. Kila Jumamosi, huwa tunaenda kutizama sinema nyumba ya sinema.

Wikendi moja, tulipokuwa tukielekea kwenye sinema, Neema akaitwa na muuzaji wa duka mzee ambaye humsumbua sana kwa sababu ya madeni ya mamake. Mimi na Mariam tukaendelea na safari tukijua Neema atatufikia. Baada ya dakika 5, tukageuka na kuona Neema akitukimbilia, na alikuwa ameshtuka. Alipokaribia kabisa akasema, “Amina, unatokwa damu!” Neema akaonyesha upande wa chini wa mwili wangu, nami nikaona doa kubwa jekundu katika nguo yangu. Nilikuwa nimeanza hedhi yangu!

Mara hiyo, nikaskia macho yangu yanachoma na machozi yakaanza kunitoka. Sikujua nilitembea kwa muda gani na doa hili kubwa. Nilitaka tu kulia, lakini mabesti wangu wakasema kuwa kama kuna mtu ambaye alikuwa ameona basi angesema kitu. “Watu wako bize sana hawana time ya kuangalia nguo yako Amina! Pia hii ni kawaida na hakuna anayeweza kukucheka”, akasema Mariam. Neema akakimbia dukani na kuleta kitambaa cha kujifunga kwenye kiuno ili kuficha nguo yangu. Kisha akaenda dukani na kuninunulia pedi.

Tulimngoja Neema chini ya mti. Wakati huo, Mariama akanieleza siri kubwa. Yeye tayari alikuwa amepata hedhi zake mieze 6 kabla. Akasema aliogopa sana mara ya kwanza lakini dadake akamhakikishia kuwa hedhi ni jambo la kawaida na hakuna haja ya kuwa na aibu.

Mimi na mabeshte zangu tukarundi nyumbani ili niweze kuvaa pedi. Nawashukuru sana marafiki zangu. Hata kuna wakati Neema aligeuka na kuniambia, “Amina. Hii ni sehemu ya kawaida ya kuwa mdada. Usijali, utakuwa sawa.” Na ni kweli – Niko sawa!