Kutoka mwanamiereka wa mtaa hadi bingwa wa dunia

Kukutana na wasichana wa Senegali ambao wanavunja kanuni!

Kutoka mwanamiereka wa mtaa hadi bingwa wa dunia

Wazazi wangu walifariki nilipokuwa mdogo, hivyo nililelewa na wanawake katika jamii yangu. Ingawa walinionyesha upendo mwingi, nilihamia nyumba moja hadi nyingine na kamwe sikuhisi kama nilitosheka na popote. Lakini, nilianza mieleka na maisha yangu yakabadilika. Hatimaye nimepata kitu ambacho naweza kusema kuwa kinanitosha.

Mwanamke maalum kijijini changu alianza mieleka Senegali miaka michache iliyopita, wakati mieleka haikuonekana kama "mchezo wa wanawake". Sambou alivunja ubaguzi wote. Alivunja kanuni zote. Katika nyakati ambazo watu walidhani mieleka ni ya wanaume pekee, Sambou aliingia uwanjani na kushangaza kila mtu. Hata alifuzu kushiriki katika Olimpiki! Ajabu sana ... mwanamke kutoka kijiji changu kidogo nchini Senegali akishindana kimataifa. Chochote kinawezekana unapokizingatia, unafikiri vipi?

Isabelle Sambou aliporudi Senegali alianzisha klabu ya mieleka kwa wasichana wadogo, kwa sababu aliamini kuwa wasichana wanaomfuata wana uwezo wa kuwa mabingwa wa dunia pia. Na hivyo ndivyo nilianza kushiriki. Nilijisajili kupata mafunzo kwa sababu, kwa hisani ya Sambou, nina ndoto kuwa siku moja nitakuwa bingwa wa dunia. Mbali na ndoto yangu, napenda mieleka kwa sababu hunifanya kujihisi mwenye nguvu na mwenye kusudi. Unahitaji kujifunza jinsi ya kujiamini na kuamini nafsi yako, vinginevyo mpinzani wako atagundua hofu yako na unaweza kupoteza shindano.

Sambou hakupata ubingwa kwa siku moja. Alianzia mtaani na kuendelea hadi kufika kileleni. Nami nafanya hivyo pia Kuogopa ndoto kubwa haitanisaidia kwa namna yoyote, hivyo nitazingatia ninavyoweza mazoezi magumu wakati wote. Pia kila asubuhi ninapoamka nafunga macho yangu na kuwaza kama mshindi wa kila shindano na kushika medali ya dhahabu. Baada ya kuwaza kama mshindi kwa mara nyingi, sasa haionekani tena kuwa ngumu.

Isabelle Sambou alifanya kijiji chetu kujivunia hadi wazee wakamfanya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa chifu na kiongozi kijijini. Na kwa sababu sasa nimegundua kwamba ndondi ndicho kitu ninachotaka kufanya maishani, nitakifuatilia kwa chochote nilicho nacho. Sitaacha kuchukua hatua na kufuata ndoto zangu kwa sababu wasichana wanapoingia ndani ya uwanja, mambo makubwa yanaweza kutendeka!