Mambo manne unayohitaji kujua kuhusu wazazi wako

Tutakufuna siri kadhaa

Mambo manne unayohitaji kujua kuhusu wazazi wako

Mungu wangu, wazazi! Tunawapenda, lakini wakati mwingine... Kama tulivyosema, Mungu wangu! Siku moja baada ya shule, mimi na marafiki zangu tulikuwa tukipiga umbeya. Na kupiga umbeya. Tulianza kuunda orodha. Orodha za mambo yote yanayoudhi ambayo wazazi wetu wanafanya yanayoharibu maisha yetu.

Ilikuwa orodha ndefu. Nilizileta kwa dada yangu mkubwa Shara. Ni nani ambaye angeelewa vyema zaidi kuliko dada yangu mkubwa?! Sivyo. Ana mtoto wa miaka miwili. Alisema kuwa ikiwa tungeunda orodha, angeunda yake binafsi. Amua anayesema ukweli.

1. Watajaribu kukuamini.
Sisi: Wanatuambia kilicho sawa au kisicho sawa. Wanauliza marafiki, nguo, muziki, vivutio... kimsingi kila kitu tulichokichagua. Dada Yangu: Wana kitu usicho nacho — tajiriba. Hawawi sahihi wakati wote, huo ni ukweli, lakini wanajua mambo mengi kuhusu maisha kuliko wewe na wanataka tu kukusaidia kufuata mkondo mzuri.

2. Ni wadadisi.
Sisi: Wanatuuliza mara kwa mara na wakati mwingine hata kukagua vitu vyetu. Inaudhi! Dada Yangu: Wana hamu ya kujua na kuvutiwa na kile kinachoendelea katika maisha yetu. Huenda akaonekana kama wasiokuamini... na ingawa huenda wakavuka mpaka, wana nia njema.

3. Wanapenda kutoa maagizo.
Sisi: Wanatekeleza amri kali ya kutotoka! Tuna kazi za kufanya nyumbani! Wana sheria nyingi sana tunazopaswa kufuata! Hawatuelewi! Dada Yangu: Wazazi wako wanajitahidi na kukupa makao na chakula. Wanastahili kushukuriwa kwa hilo.

4. Wanakupenda sana.
Sisi: Sawa, lakini... Dada Yangu: Mama yako alipitia machungu ya ujauzito ili kukuzaa na familia yako imejitolea kwa kila hali kukuona ukikua na kuendelea vyema. Kila kitu wanachofanya, hata kama kinaonekana kuudhi, kibaya, kisichofaa au kisicho sahihi, ni kukusaidia kuwa bora na kuepuka kuumia. Huenda kisiwe kitu kinachofaa wakati wote lakini moyo wao upo mahali panapofaa.