Kutafuta kabila lako

Usipitie maisha peke yako... tafuta baadhi ya marafiki wazuri wa kuwategemea

Kutafuta kabila lako

Marafiki zangu katika mtaa wangu mpya ni wazuri. Wako hapa kwa ajili yangu kila wakati, na ninaweza kuwategemea wakati wowote ninahitaji kitu chochote. Hata hivyo, miaka michache iliyopita sikuwa na kundi hili la marafiki. Niliishi mahali pengine na nilikuwa na marafiki ambao hawakuwa wazuri. Nilipohama, nilifurahi kuwa na mwanzo mpya lakini mchakato wa kupata marafiki wapya ulikuwa ukichokesha. Hivi ndivyo nilivyofanya ili kupata marafiki zangu:

Kuwa wewe mwenyewe, hakuna mwingine kama wewe

Nikiwa na marafiki zangu wa zamani nilijifanya kuwa mtu mwingine ili niweze kufaa. Hiyo ilinifanya niwe katika matatizo mengi kwa sababu niliona kuwa vigumu kusema HAPANA kwa mambo. Kwa hivyo wakati huu nikaamua kuwa mimi mwenyewe. Nilifanya nilichofurahia na mimi mwenyewe nikajitoteza! Rafiki yangu Temi, nilikutana na yeye katika klabu ya maskauti ya wasichana na akanipenda jinsi nilivyo! Sasa yuko kwenye timu yangu na ananisaidia sana wakati nitahitaji msaada.

Watafute watu wanaofikiria na kutenda kama wewe.

Kupata marafiki na watu ambao wana maadili, vivutio na mapendeleo sawa na wewe ni mahali pazuri pa kuanzia. Kama vile rafiki yangu Simi, nilikutana na yeye kwa watengeneza nywele, Wimbo wa Beyonce ulianza kuiamba na wote tukaanza kuimba na kucheza. Mwishowe tulitembea pamoja kwenda nyumbani kutoka kwa watengeneza nywele na alinifunza mengi sana. Sio kuhusu Beyonce pekee bali pia anapenda kujitolea. Alinionyesha mpango anaoendesha wa kuwasaidia akina mama wachanga. Kwa pamoja tumefanya mpango wa kubadilisha jamii yetu. #girlpower

Kuwa mjasiri, kuwa wa kwanza

Siku moja nikiwa njiani kwenda nyumbani kulikuwa na wavulani kwenye kona waliokuwa wakiwanyanyasa watu walipokuwa wakitembea. Nilikuwa na wasiwasi kutembea karibu nao hadi nilipomwona msichana mmoja akitembea. Wakati wavulana walipomwita kwa jina alijitetea. Nilipendezwa na ujasiri wake kwa hivyo nikamfuata ili kuomba ushauri. Wakati mwingine lazima uwe mjasiri na uwaombe watu ushauri unaohitaji. Usiifikirie sana au uwe mwoga. Hesabu kuanzia 5, 4, 3, 2, 1 kichwani mwako na uende useme hujambo na ujitambulishe. Hivyo ndivyo nilivyofanya na Dada na sasa amenipa ushauri mwingi kuhusu jinsi ya kujitetea. Yeye ni rafiki yule ambaye ninaweza mtegemea kila wakati. Hebu fikiria kama singeenda alipokuwa? Hatungekuwa marafiki leo!

Kisha nikawatambulisha Temi, Simi na Dada na BOOM! Kundi langu kuu likabuniwa! Wakati wowote ninahisi upweke ninawapigia simu na hao hunifanya nihisi vizuri. Iwapo nina tatizo, ninajia watakuwa kunisaidia. Hivyo ndivyo marafiki wema hufanya. Iwapo hujatapa kundi lako bado basi usiwe na wasiwasi... kumbuka urafiki mwema huchukua muda kukua. Usife moyo - kama ninaweza pia wewe unaweza!