Je, huyu kijana anakupenda?

Jinsi ya kujua ishara

Je, huyu kijana anakupenda?

Huwa unakosa usingizi ukiwaza mtu fulani? Huwa unajiuliza ikiwa yeye hukuwaza pia? Sote tumepitia hapo. Na ni kawaida sana kuwaza kuhusu wakaka tunapoendelea kuwa wakubwa. Hii ni sehemu ya ubalehe na utu mzima.

Kama rafiki yangu Sarah. Alimpenda kijana mmoja aliyeitwa TJ. Lakini aliogopa kuwa wa kwanza kuzungumza naye. Sarah ni aina ya watu ambao hutaka kujitayarisha kabisa kabla ya kufanya jambo. Walipoongea mara ya mwisho, Sarah alihisi poa kuhusu TJ lakini bado alitaka mawaidha kutoka kwa dadake mkubwa ili kujihakikisha.

Hapa ni mazungumzo baina ya Sarah na TJ:

TJ - Wow Sarah, umebadilisha mtindo wako wa nywele, Napenda hiyo braid yako. Ninaipenda zaidi ya mtindo wa nywele uliopita.

Sarah – Asante! Siku nyingi hatujaonana.

TJ – Ndio, Imekuwa muda mrefu. Nilimwambia besti yangu jana kuhusu wewe. Na pia vile namiss kuwa na wewe.

Sarah – Oh hio ni poa. Umekuwa ukifanya nini?

TJ – Hakuna hata. Ninacheki ile series uliniambia. Naipenda! Unaeza kuja tuwatch episode inayofuata pamoja?

Baada ya Sarah kusema na dada yake vile waliongea, dadake akamweleza vile anaweza jua kama chali anampenda au la. Alisema hivi:

  1. Kama kijana anaangalia sana juu ya mwonekano wako, labda anakupenda. Hasa akikumbuka vile ulikuwa unaonekana zamani. TJ anakumbuka mitindo yote ya nywele ya Sarah.
  2. Kama kijana anaambia mabesti wake kukuhusu, anaweza kukupenda Anawaambia sababu anataka wakutane na wewe.
  3. Kama kijana anavutiwa na mambo wewe huwa unafanya, basi anaweza kukupenda. TJ anakumbuka series ambayo Saraha alitaja na hata akaanza kuitizama. Anataka kufurahia yale mambo Sarah anafurahia.
  4. Pia, TJ anataka kumwalika watazame pamoja. Kijana anayekupenda hutaka mfanye jambo pamoja.

Kutokana na mawaidha haya kutoka kwa dadake, Sarah akaamua kumweleza TJ vile alikuwa anahisi. Bahati nzuri, TJ akasema anahisi vile vile pia! YAY, Wapendanao Sarah na TJ!

Hata kama huna dada mkubwa kama Sarah, unaweza kuongea na wasichana wengine katika jamii unayoishi kama una swali lolote!