Kuwa Miss Independent – Sehemu ya 1

Inaanza na wewe!

Kuwa Miss Independent – Sehemu ya 1

Vipi dada,

Jina langu ni Tanya. Nina miaka 17 na ninachokitaka sana maishani ni kuweza kujitegemea. Nilikuwa na maisha mazuri. Nilienda shule, nilikuwa na chakula na nguo za kuvaa, lakini baba yangu alipopoteza kazi mambo yalibadilika na kuwa mabaya. Nililazimika kuwacha shule kwa sababu hakuweza kulipa karo yangu.

Kuwacha shule haikuwa rahisi kwangu. Nilihisi nililazimika kuwacha ndoto zangu za kujitegemea, kwa sababu bila masomo nilihisi ingekuwa vigumu kutimiza ndoto zangu. Siku moja nilikuwa nimeketi chumbani changu nikisoma hadithi kwenye Springster nilipobofya hadithi inayoitwa Kuwa Bosi Wako Mwenyewe. Ilikuwa nilichohitaji kusoma kwa wakati ule.

Kupitia hadithi ile, niligundua kwamba ningeweza kuanza biashara yangu mwenyewe na nijitegemee. Masomo sio njia pekee. Lakini ili kuanza safari hii nilihitajika kubadilisha mtazamo wangu na nilivyokuwa nikihisi.

Hatua ya kwanza kuwa Miss independent ni kujiamini na kuamini uwezo wako wa kutimiza ndoto zako. Najua wakati mwingine ni vigumu kujiamini wakati mambo yote karibu nawe yanaenda mrama, lakini usisisitize hayo. Badala yake, hapa kuna mambo mawili unafaa kufanya:

Kuwa na fikra nzuri

Wanasayansi wanasema kuwa asilimia 70 ya fikra zetu ni mbaya. Je, ulijua? Na nyanyangu daima aliniambia, “Mawazo mbaya hayawezi kukupa maisha mazuri.” Anajua vyema. Ili kujitegemea lazima uwache mawazo mabaya na uwe na mawazo mazuri.

Fahamu ujuzi na talanta zako

Nilikuwa nafanya vyema shuleni, lakini kwa sababu niliwacha shule haimaanishi niliwacha kuwa mwerevu. Kama nilikuwa sawa katika hesabu shuleni, ninaweza pia kuwa sawa katika hesabu za kuendesha biashara. Ni vyema kujua mambo unayomudu vizuri. Itakufanya ujiamini zaidi.

Daima kumbuka kuwa mawazo yako huongoza hisia zako na hisia zako zinaongoza maamuzi unayofanya na hatua unazochukua. Kwa hivyo kabla ya kuweza kujitegemea ni lazima kwanza uwaze kuwa inawezekana kwako. Na wajua vipi dada? Inawezekana.

Nenda hadi chini ili upate maelezo zaidi kuhusu safari yangu ya kuwa huru Sehemu ya 2, au andika Kuwa Miss Independent – Sehemu ya 2 kwenye sehemu ya tafuta.