Njia 3 za kukabiliana na uchovu wa likizo

Jaribu shughuli hizi za kufurahisha!

Njia 3 za kukabiliana na uchovu wa likizo

Jina langu ni Caroline na sikufurahia sana shule zilipofungwa kwa sababu sikuwa na jambo lolote la kufurahisha la kufanya isipokuwa kumsaidia mama yangu – jambo ambalo linachosha! kwa bahati nzuri, likizo hii binamu yangu ninaye mpenda sana Maria alikuja kututembelea. Yeye ni mwenye wingi wa nguvu na alinionyesha jinsi ninavyoweza kutumia ubunifu wangu kupata njia za kujiburudisha mimi na familia yangu.

Tengeneza kitabu cha historia ya familia yako

Jambo tulilofanya la kwanza ni kutengeneza kitabu kilichokuwa na hadithi za kupendeza za familia yetu. Nyanya wetu alifariki miezi 6 iliyopita na Maria alihisi kwamba hii ingekuwa njia bora ya kuhakikisha hatutasahau hadithi zote alizotusimulia. Kwa hiyo, tulitumia karatasi kutoka kwa vitabu vyetu vya shule na kalamu ya bluu na nyeusi tulizopata ndani ya nyumba. Tulipomaliza hadithi zile, tulitoboa mashimo mwishoni wa karatasi zile na tukaweka uzi ili kuunganisha kurasa zile pamoja. Waona, ni rahisi sana! Kwa nini na wewe usitengeneze?

Cheza mchezo wa herufi

Maria pia alinifunza mchezo wa herufi; unapaswa kutaja kitu kinachoanza na kila herufi, kuanzia mwanzo hadi mwisho. Lakini ujanja uko hapa; kila kitu unachokitaja lazima kiwe na mada sawa – kwa hiyo aina ya vyakula, waimbaji, mambo ya historia nk. Tulicheza mchezo huu mara kadhaa na mada tofauti hadi nikamwomba mama yangu ajaribu mchezo huo!

Toa msaada

Kuna mambo machache yenye kuridhisha kuliko kumsaidia mtu anayehitaji usaidizi. Kwa hiyo, tulijitolea tukiwa na Maria masaa kadhaa kila wiki kwenye kitu cha jamii kilicho mtaani kusaidia watu wazima kusoma na kuandika. Nilihisi vizuri sana kuwa wa msaada kwa majirani zangu na kuwasaidia kusoma na kuandika.

Bila shaka, sasa ninapenda likizo sana kwa sababu zinanipa muda wa kufanya mambo mapya ambayo kwa kawaida huwa nakosa muda wa kufanya. Na shukrani zote ni kwa binamu yangu Maria, aliyenitia moyo kutumia ubunifu wangu na rasilimali zilizo karibu nami!