Sheria na Masharti

Asante kwa kutembelea Springster! Sisi ni Girl Effect na tunaendesha Springster Sisi ni shirika la msaada, lililo na makao Uingereza, na tunafanya kazi ili kuwapa uwezo wasichana kama wewe. Anwani na maelezo mengine yetu yanaweza kupatikana chini ya kanuni hizi.

Tafadhali hakikisha umesoma na unafuata kanuni hizi. Si kanuni za kukuzuia kufurahia - lakini ni za kuhakikisha kila mtu ako salama na anatumia Springster kwa njia mwafaka!

Kuwa huru kuwasiliana nasi kwa maswali au maoni yoyote kwa kutuandikia barua pepe springster@girleffect.org. Tunapenda kusikia kutoka kwako!

KANUNI

1). Tunaweza kufanya mabadiliko kwa kanuni hizi mara kwa mara. Tafadhali hakikisha unafahamu toleo la hivi karibuni kwa kuangalia hapa tena. Tunaweza pia kubadilisha Springster, ikiwa ni pamoja na kuifunga kwa muda mfupi, ili kuboresha hisia zako. Tutajitahidi kukujulisha mapema, lakini hii inaweza kukosa kuwezekana wakati mwingine.

2). Springster inalenga watu wa kati ya umri wa miaka 13 – 24. Ikiwa una umri wa chini ya 13, tafadhali usitumie Springster, kwani haitakufaa. Ikiwa una umri wa chini ya 16, tafadhali hakikisha kwanza kuwa umepata idhini kutoka kwa mzazi au mlezi wako kabla ya kutumia Springster.

3). Unapotumia Springster, tutakusanya maelezo ya kibinafsi kutoka kwako. Tafadhali soma Sera yetu ya Faragha ili kufahamu:

  • Ni maelezo yapi tunakusanya;
  • Jinsi tunavyokusanya;
  • Jinsi tunavyoyatumia; na
  • Jinsi unavyoweza kupata maelezo zaidi.

4). Kunaweza kuwa na upatikanaji wa maelezo kuhusu afya katika Springster. Maelezo haya si mbadala wa ushauri wa kimatibabu. Ikiwa una maswali au wasiwasi fulani kuhusu afya yako, tafadhali tembelea kwa daktari au mtaalamu mwingine wa afya.

5). Springster ni jamii, hii ina maana kwamba pamoja na maudhui tunayotoa katika Springster, pia wewe unaweza kutoa maudhui yako mwenyewe. Hii inaweza kujumuisha maoni, blogu, twiti, podikasti, mazungumzo na faili za sauti-picha. Kabla ya kutuma maudhui, tafadhali hakikisha:

  • Huna shida kushiriki maudhui na Girl Effect na watumiaji wengine wa Springster. Hii ni muhimu hasa ikiwa maelezo haya ni ya kibinafsi;
  • Ikiwa utataja wengine, kuwa na ruhusa ya kushiriki maelezo yao kwenye Springster. Hii ni muhimu hasa ikiwa maelezo haya ni ya kibinafsi
  • Maudhui ni kazi yako mwenyewe na haujainakili kutoka mahali pengine. Lazima uwe na ruhusa ya kutumia maudhui ya watu wengine (kwa mfano, nyimbo au video);
  • Maudhui haijumuishi uwongo wowote au ukweli usio sahihi; na
  • Una furaha ikiwa tutatumia maudhui kwa ajili ya Springster, pamoja na shughuli zingine za Girl Effect (kwa mfano, tunapoelezea kuhusu kazi tunayofanya pamoja na wengine).

6). Kunaweza kuwa na viungo vinavyokuunganisha na tovuti na mashirika mengine kwenye Springster. Kanuni hizi hazitatumika kwa tovuti hizo na unapaswa kuangalia kanuni kwenye kila tovuti wakati unaipofikia, kwani hatuwezi kuwajibika kwa ajili ya mashirika mengine.

7). Ikiwa utajisajili-kama mshirika (au “Mwana Springster” kama tunavyopenda kukuita!), utapaswa kuingia na kuwa na nenosiri. Hifadhi maelezo haya kwa usiri kwani hutaki mtu mwingine kuingia kwenye Springster yako na kujifanya kuwa wewe! Tunatarajia kuwa kama mshirika utawajibika kwa ajili ya shughuli zako.

8). Tunaweza kuomba maoni yako katika tafiti. Tafadhali shiriki ikiwa tu unataka, tafiti si za lazima. Tunafanya hivyo ili kuelewa vizuri jinsi unavyotumia tovuti, na kutoa maudhui muhimu zaidi kwako (na watumiaji wengine wa Springster). Tunaweza kushiriki matokeo na wengine, lakini hii haitajumuisha maelezo yako ya kibinafsi isipokuwa ikiwa tumekuarifu kwa uwazi vinginevyo.

9). Tunajitahidi kuhakikisha kuwa Springster ni salama kuitumia, lakini hatuwezi kuthibitisha kuwa ni salama kutokana na virusi vyovyote vya kompyuta au msimbo wa uharibifu. Hatutawajibika kwa uharibifu wowote kwenye simu yako ambao unaweza kutokana na matumizi ya Springster.

10). Tunajitahidi kuweka Springster kuwa salama na kupatikana kwa watumiaji wote. Ili kutusaidia, tafadhali usijaribu kufanya udukuzi kwa Springster, kuweka virusi au kufanya kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuidhuru Springster.

11). Jina "Springster", alama yetu kuu na ubunifu wa jukwaa zinamilikiwa na Girl Effect. Tafadhali omba idhini yetu kabla ya kutumia yoyote ya haya kwa sababu yoyote (tofauti na kutumia Springster).

12). Springster inalenga matumizi yako ya kibinafsi tu. Ikiwa wewe ni shirika la kibiashara, tafadhali usitumie Springster, kwani maudhui hayalengi kutumika na wewe na huna haki ya kutumia maelezo haya.

13). Ikiwa kwa wakati wowote utavunja mojawapo ya kanuni hizi, tunaweza (kati ya vitendo vingine) kukuzuia kutumia Springster katika siku za baadaye.

14). Ikiwa una lalamiko, au ikiwa una wasiwasi kuhusu chochote katika Springster, tafadhali sema na kuwasiliana nasi kupitia barua pepe: springster@girleffect.org

Tunatumai utafurahia kuwa sehemu ya jamii ya Springster!

Girl Effect ni kampuni ya ukomo na shirika la msaada lililosajiliwa Uingereza, UK. Anwani ya usajili ni Ingeni Building, 17 Broadwick Street, London W1F 0AX. Namba ya kampuni ni 07516619 na namba ya usajili kama shirika la msaada ni 1141155.