Kuhusu Springster

Karibu Springster! Eneo la wasichana kuungana, kujifunza na kujithamini!

Jiamini kwa sababu tayari tunafanya...

Pia tuna msimbo wa Springster, mwongozo wa maisha wa kutusaidia sote kuwa bora zaidi!

Msimbo wa Springster*

1 Kila Mtu ni Springster.
Hakuna sheria za anayeweza wala asiyeweza kuwa Springster. Kila mtu ana uhuru wa kujiunga.

2 Pamoja Kila Wakati. Huwi peke yako kamwe. Tunaweza kutegemeana hata nini kitokee kwa sababu hilo ndilo Springsters hufanya.

3 Shiriki upendo.
Usione soni! Shiriki hadithi yako! Tupo hapa kusaidia na kusherehekea kila mmoja wala si kuhukumu.

4 Endelea kuamini.
Nyakati zinapokuwa ngumu tunapata usaidizi kutoka kwa marafiki, familia na jamii - hatukati tamaa.

5 Jitahidi.
Hakuna mbinu ya muujiza ya ufanisi. Inahusisha jitihada na kuwa na mpango.

6 Ondoa vizuizi.
Usimruhusu yeyote kukuwekea mipaka ya kile unachoweza kufaulu kufanya maishani

7 Onekana Mjinga
“Jitihada ni Muhimu. Lakini usisahahu kufurahia pia"

#8 Ukiwa Springster utakuwa Springster milele.*
Wewe ni Springster daima. Haijalishi unakoenda, mlango uko wazi wakati wote.

Shiriki msimbo wa Springster